Immature | |
---|---|
![]() | |
Taarifa za awali | |
Pia anajulikana kama | IMx |
Amezaliwa | Los Angeles, California, U.S. |
Miaka ya kazi | 1990–2002, 2009–present |
Studio | |
Ameshirikiana na | |
Wavuti | http://immatureofficial.com/ |
Wanachama | |
Marques Houston Jerome Jones Kelton Kessee | |
Don Santos |
Immature (baadaye wakafahamika kama IMx) ni kundi la vijana la muziki wa R&B kutoka nchini Marekani. Kundi linasimamiwa na mtayarishaji wa rekodi Chris Stokes.
Wanachama wake ni pamoja na Marques "Batman" Houston (amezaliwa Agosti 4, 1981), Jerome "Romeo" Jones (amezaliwa Oktoba 25, 1981), na Kelton "LDB" Kessee (amezaliwa Januari 2, 1981), wote wakiwa wazawa wa Los Angeles, California, mahali ambapo ndipo kundi lilipoanzishwa.
Kundi limetoa albamu nne chini ya mwamvuri wa jina la Immature. Albamu hizo ni pamoja na: On Our Worst Behavior (1992; albamu pekee iliyohusisha mwanachama wa awali Don "Half Pint" Santos, baadaye nafasi yake ikachukuliwa na Kessee), Playtyme Is Over (1994), We Got It (1995) na The Journey (1997).
Ilipotimu mwaka wa 1999, kundi likabadili jina lao na kuwa IMx. Ilipotimu miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, wakatoa albamu mbili. Nazo ni Introducing IMx na IMx, vilevile wakatoa albamu yenye vibao mseto vilivyotamba yenye jina la Greatest Hits mnamo mwaka wa 2001.[1]
Kundi pia likajutupa katika uwanja wa tasnia ya maigizo. Wakashiriki katika filamu kama vile House Party 3 na House Party 4: Down to the Last Minute) na upande wa runinga walikuwemo kwenye A Different World, Sister, Sister, Family Matters, Soul Train na All That) kabla ya kila mtu kwenda safari yake mnamo mwaka wa 2002.
Mwaka wa 2010, Houston alitangaza kupitia kipindi cha runinga cha hip hop & R&B cha 106 & Park kwamba kundi linapanga kurekodi albamu nyingine itoke mwaka wa 2011. Baadaye wakatoa taarifa ya albamu kuwa jikoni kwa jina la "Forever Immature." Ilipangwa kutolewa katika majira ya joto ya mwaka wa 2013, ikiwa pamoja na ziara, walakini, tarehe ya kutolewa haikutolewa kwa mradi huo. Mnamo tarehe 6 Novembea, 2013, Immature walitumbuiza onyesho lao la kwanza tangu warudi tena mzigoni katika ukumbi wa Club Nokia jijini Los Angeles wakiwa na bendi nyingine Next na Dru Hill.
Mnamo mwezi wa Septemba 2019, Immature walitangaza ziara yao iliyopewa jina la #TBTour wakisindikizwa na Ray J, B5 a J. Holiday.[2]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)