| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Bhinneka Tunggal Ika (Kijava/Kikawi: Umoja katika tofauti) Itikadi: Pancasila | |||||
Wimbo wa taifa: Indonesia Raya | |||||
Mji mkuu | Jakarta | ||||
Mji mkubwa nchini | Jakarta | ||||
Lugha rasmi | Kiindonesia | ||||
Serikali | Jamhuri Prabowo Subianto Gibran Rakabuming Raka | ||||
Uhuru Kutangaza Kutambuliwa |
Kutoka Uholanzi 17 Agosti 1945 27 Desemba 1949 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,904,569 km² (16th) 4.85% | ||||
Idadi ya watu - 2015 kadirio - 2011 sensa - Msongamano wa watu |
255,461,700 (4th) 237,424,363 124.66/km² (84th) | ||||
Fedha | Rupiah (IDR )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
various (UTC+7 to +9) not observed (UTC+7 to +9) | ||||
Intaneti TLD | .id | ||||
Kodi ya simu | +62
- |
Indonesia ni nchi ya visiwa katika Asia ya Kusini-Mashariki. Iko upande wa Kusini-Mashariki kati ya Bahari ya Uhindi na Pasifiki.
Visiwa vyake ni sehemu ya Funguvisiwa la Malay, ingawa Guinea Mpya kwa kawaida haihesabiwi katika fungu hilo.
Indonesia imepakana na Papua Guinea Mpya kwenye kisiwa cha Guinea Mpya, pia na Timor ya Mashariki kwenye kisiwa cha Timor, halafu na Malaysia kwenye kisiwa cha Borneo.
Nchi nyingine zilizo karibu ni Australia, Singapur na Ufilipino.