Isimu amali

Isimu amali ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchambuzi na uchanganuzi wa lugha kupitia kwa maoni ya mtumiaji wa lugha husika. Hasa taaluma hiyo inachunguza uchaguzi wa miundo wa maneno anaoufanya msemaji, vikwazo vya kijamii msemaji anavyokabiliana navyo katika matumizi yake ya lugha, na athari nyingine za kijamii za matumizi ya lugha. Wengine hudai kuwa taaluma hiyo ni sehemu ya isimujamii.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne