Jada Pinkett Smith | |
---|---|
![]() Pinkett Smith kwenye NY PaleyFest 2014 kwa ajili ya Gotham | |
Amezaliwa | Jada Koren Pinkett 18 Septemba 1971 |
Majina mengine | Jada Koren (with Wicked Wisdom) |
Kazi yake | Mwigizaji, mtunzi wa nyimbo-mwimbaji, mfanyabiashara |
Miaka ya kazi | 1990–hadi sasa |
Ndoa | Will Smith (m. 1997–present) |
Watoto | Jaden and Willow |
Tovuti | |
jadapinkettsmith.com |
Jada Koren Pinkett Smith (/ˌdʒeɪdə ˌpɪŋkɨt ˈsmɪθ/; amezaliwa na jina la Jada Koren Pinkett; mnamo Septemba 18, 1971)[1] ni mwigizaji wa filamu, mtunzi-mwimbaji wa nyimbo, na mfanyabiashara kutoka nchi ya Marekani. Alianza shughuli zake mnamo 1990, wakati alipofanya uhusika wa kualikwa katika ucheshi uliodumu kiasi True Colors. Amecheza katika filamu ya vichekesho A Different World, iliyotayarishwa na Bill Cosby, na pia akashiriki pamoja na Eddie Murphy kwenye filamu ya The Nutty Professor (1996). Ameshiriki filamu za maigizo kama vile Menace II Society (1993) na Set It Off (1996). Ameonekana katika filamu zaidi ya 20 za mitindo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Scream 2, Ali, The Matrix Reloaded, The Matrix Revolutions, Madagascar, Madagascar: Escape 2 Africa, na Madagascar 3: Europe's Most Wanted.
Mwaka wa 1997, aliolewa na rapa na mwigizaji Will Smith. Wana watoto wawili, Jaden na Willow. Wawili hawa wameanzisha Will and Jada Smith Family Foundation, asasi ya kutoa misaada inayotazamia hasa vijana waishio mijini ili waweze kujikimu na vilevile wanafanya kazi na asasi zingine zisizo za kiserikali kama vile YouthBuild na Lupus Foundation of America.