Jalisco

Puerto Vallarta, Jalisco
Bendera ya Jalisco
Mahali pa Jalisco katika Mexiko

Jalisco (kwa Kinahuatl: tambarare ya mchanga) ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexico ya kati-magharibi ya nchi. Ina pwani na Pasifiki. Mji mkuu na mji mkubwa ni Guadalajara.

Imepakana na Nayarit, Zacatecas, Aguascalientes, San Luis Potosí, Guanajuato, Colima na Michoacán.

Jimbo lina wakazi wapatao 7,000,000 (2005) wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 79,085.

Gavana wa jimbo ni Emilio González Márquez.

Lugha rasmi ni Kihispania.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne