Jamhuri

Aina za jamhuri duniani
*Nyekundu - Serikali ya kiraisi
*Kijani - Serikali ya raisi pamoja na athira kubwa ya bunge
*Kijani-kizeituni - Serikali ya kiraisi pamoja na waziri mkuu
*Machungwa - Serikali ya kibunge
*Kahawiya - Jamhuri zinazoruhusu chama kimoja pekee
Mengine: Ufalme au serikali ya kijeshi
Angalizi: Nchi mbalimbali zinazojiita "jamhuri" hutazamiwa na wengine kama udikteta. Ramani inaonyesha hali ya kisheria si hali halisi.

Jamhuri inataja aina za serikali zisizo na mfalme, malkia, sultani au mtemi wowote.

Mara nyingi wananchi humchagua kiongozi wao akiitwa mara nyingi rais. Kuna pia vyeo vingine.

Katika nadharia jamhuri inatakiwa kufuata muundo wa demokrasia. Lakini kuna pia jamhuri pasipo na serikali inayochaguliwa zikifuata kwa mfano muundo wa udikteta au utawala wa kijeshi.

Kinyume chake kuna pia muundo wa ufalme pamoja na demokrasia, kwa mfano Uingereza au Uswidi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne