Jason Statham

Jason Statham
Jason Statham
Jason Statham
Jina la kuzaliwa Jason Statham
Alizaliwa 26 Julai 1967
Uingereza
Kazi yake Mwigizaji
Mwanamitindo
Mwogeleaji

Jason Statham (amezaliwa 26 Julai 1967) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Uingereza. Anafahamika zaidi kwa kucheza kama Bacon katika filamu ya Lock, Stock and Two Smoking Barrels, Jake Green katika filamu ya Revolver, Turkish katika filamu ya Snatch.

Pia Statham amepata kuonekana katika filmu nyingi sana za Kimarekani. Filamu hizo ni kama vile The Italian Job, Crank, The One na War ambazo zote alicheza na miwgizaji filamu mashuhuri wa Kichina Jet Li. Vilevile katika The Transporter, humo alicheza kama nyota kiongozi wa filamu hiyo na inaamika kwamba ile ndiyo iliyomfanya aonekane zaidi kwa watu wa Marekani.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne