Jay-Z | |
---|---|
![]() Jay-Z, mnamo 2011
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Shawn Corey Carter |
Amezaliwa | 4 Desemba 1969 Brooklyn, New York, Marekani |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Rapa, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 1986 – hadi |
Studio | Roc Nation/Atlantic Records |
Ame/Wameshirikiana na | Jaz-O, Memphis Bleek, Beanie Sigel, Amil, Beyoncé, Linkin Park, Kanye West, R. Kelly, T.I., UGK, Lil Wayne, Freeway, The Notorious B.I.G., Nas, Sean Combs, Foxy Brown, Pharrell, Coldplay, Eminem |
Tovuti | www.jay-z.com |
Shawn Corey Carter (amezaliwa tar. 4 Desemba 1969[1]) ni msanii wa hip hop na mfanyabiashara kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Jay-Z. Huyu ni Ofisa Mkuu wa zamani wa Def Jam Recordings[2] na Roc-A-Fella Records.
Pia ni mmoja kati ya wanaomiliki klabu ya The 40/40 Club na New Jersey Nets. Huyu ni mmoja kati ya wasanii na mjasiriamali wa hip hop wa Marekani wenye mafanikio makubwa kabisa,[3] kwa kuuza nakala zaidi ya milioni 26 nchini Marekani na kupokea Tuzo za Grammy kadhaa kwa kazi zake za kimuziki.[4]
Pamoja na kuwa na mafanikio yake makubwa ya kimuziki, Jay-Z anafahamika zaidi kwa kujihusisha na masuala ya ugomvi na baadhi ya wasanii wengine wa soko zima la rap, moiongoni mwa ugomvi mkubwa uliokuwa unajulikana na watu wengi duniani ni ule wa yeye na rapa mwenziwe wa mjini New York Bw. Nas, ambao ulikuja kusuluishwa mnamo mwaka wa 2005.
Jay-Z alitoa albamu yake ya kwanza iliitwa Reasonable Doubt, ilipewa sifa na Rolling Stone kama albamu #248 ikiwa kama "Albamu Kali 500 za Karne". Albamu yake iliyompa sifa zaidi ni ile ya The Blueprint, iliandikwa kwa siku mbili tu, basi.[5]
Baada ya kujitangaza kwamba anastaafu muziki mnamo mwaka wa 2003, alirejea tena kazini mwishoni mwa mwaka wa 2006 na albamu yake ya Kingdom Come, ambayo iliuza kopi 680,000 katika wiki ya kwanza, na kuifanya iwe albamu ya Jay-Z iliofanya mauzo ya juu katika kipindi cha wiki ya kwanza.[6]
MTV wamemwita kama msanii wa kwanza katika orodha ya Ma-MC wao wa karne. Mnamo mwezi wa Aprili 2008, Jay-Z ameripotiwa kwenye verge kwamba ameingia ubia na Live Nation kwa kaisi cha Dola za Kimarekani zipatazo milioni 150—ambapo ni miongoni mwa mikataba mikubwa sana na ghari kwa wasanii wambo waliowahi kuungana nao.[7]
Carter amemwoa Bi. Beyoncé Knowles mnamo tar. 4 Aprili 2008.[8]
{{cite news}}
: Cite has empty unknown parameter: |coauthors=
(help)