Jeradi wa Toul

Picha yake katika kanisa kuu la Toul.

Jeradi wa Toul (pia: Gerhard, Geraud; Koln, Ujerumani, 935 hivi; Toul, leo nchini Ufaransa, 23 Aprili 994[1][2]) alikuwa askofu wa mji huo kwa miaka 31, aliyetunga sheria bora akitetea haki na uhuru wa Kanisa dhidi ya serikali, akisaidia kiroho na kimwili fukara na monasteri, pamoja na kuzuia kwa sala na saumu uenezi wa tauni [1][2][3][4].

Papa Leo IX alimtangaza mtakatifu tarehe 21 Oktoba 1050.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Aprili[5].

  1. 1.0 1.1 "Saint Gerard of Toul". Saints SQPN. 24 Aprili 2017. Iliwekwa mnamo 4 Oktoba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Gerard of Toul, St.". New Catholic Encyclopedia. Encyclopedia.com. 2003. Iliwekwa mnamo 4 Oktoba 2017.{{cite encyclopedia}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "St. Gerard, Bishop of Toul". Catholic Online. Iliwekwa mnamo 4 Oktoba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. http://www.santiebeati.it/dettaglio/50580
  5. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne