Jeremy Cronin

Jeremy Cronin (amezaliwa 12 Septemba 1949) ni mwandishi, mwanaharakati na mwanasiasa wa Afrika Kusini. Mwaka wa 1976 alitiwa ndani kwa sababu ya upinzani wake dhidi ya ubaguzi wa rangi. Kitabu chake cha mashairi Inside kilitolewa aliporuhusiwa 1983. Baada ya sera za apartheid kupinduliwa, alikuwa mwanachama wa serikali na kuwa Waziri Kaimu wa Usafiri.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne