Jibondo ni kata ya Wilaya ya Mafia katika Mkoa wa Pwani, Tanzania, yenye postikodi namba 61705.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 4,333 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,729 [2] walioishi humo.
Kata ya Jibondo inajumlisha visiwa vidogo vya Juani, Jibondo na Chole. Idadi kubwa ya wakazi wako Jibondo.
Watu hutegemea hasa uvuvi pamoja na kilimo kilichopo hasa Chole. Maji matamu hayapatikani kwenye visiwa hivi: ni lazima kuyabeba kila siku kutoka kisiwa kikuu cha Mafia isipokuwa wakati wa mvua ambako maji ya mvua hukusanywa. Chole imeunganishwa sasa na maji ya bomba kutoka Utende (kata ya Kiegeani) kwenye kisiwa cha Mafia.