Jimbo Katoliki la Lindi (kwa Kilatini "Dioecesis Lindiensis") ni jimbo la Kanisa Katoliki lenye makao makuu mjini Lindi katika kanda ya Songea upande wa kusini nchi Tanzania.
Kama majimbo yote 34 ya nchi hiyo, linafuata mapokeo ya Roma.
Eneo la jimbo lina kilometa mraba 56,060, ambapo wanaishi wakazi 791.306 (2004), wengi wao wakiwa Waislamu. Kati yao Wakatoliki ni 128.438, sawa na asilimia 16.2, nao wanaunda parokia 26.
Askofu wa jimbo ni Bruno Pius Ngonyani. Mapadri ni 51, ambao kati yao 48 ni wanajimbo na 3 watawa. Kwa wastani kila padri anahudumia waamini 2,518.