Jimbo Kuu la Bukavu (kwa Kilatini Archidioecesis Bukavuensis) ni mojawapo kati ya majimbo 47 ya Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma kadiri ya utamadunisho maalumu.
Kikanisa lina majimbo ya Butembo-Beni, Goma, Kasongo, Kindu na Uvira chini yake.
Askofu mkuu wake ni Francois-Xavier Maroy Rusengo.