Jimbo Katoliki la Mtwara (kwa Kilatini "Dioecesis Mtuarana") ni jimbo la Kanisa Katoliki lenye makao makuu mjini Mtwara katika kanda ya Songea upande wa kusini nchi Tanzania.
Kama majimbo yote 34 ya nchi hiyo, linafuata mapokeo ya Roma.
Eneo la jimbo lina kilometa mraba 7,780, ambapo wanaishi wakazi 859,000 (2013), wengi wao wakiwa Waislamu. Kati yao Wakatoliki ni 73,700, sawa na asilimia 8.6, nao wanaunda parokia 18.
Askofu wa jimbo ni Titus Joseph Mdoe. Mapadri ni 42, ambao kati yao 23 ni wanajimbo na 19 watawa. Kwa wastani kila padri anahudumia waamini 1.754.