Jimbo Kuu la Juba (kwa Kilatini Archidioecesis Iubaensis) ni mojawapo kati ya majimbo 7 ya Kanisa Katoliki nchini Sudan Kusini na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Malakal, Rumbek, Tombura-Yambio, Torit, Wau na Yei.
Askofu mkuu wake ni Stephen Ameyu Martin Mulla.