Jimbo Kuu la Kinshasa (kwa Kilatini Archidioecesis Kinshasana) ni mojawapo kati ya majimbo 47 ya Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma kadiri ya utamadunisho maalumu.
Kikanisa lina majimbo ya Boma, Idiofa, Inongo, Kenge, Kikwit, Kisantu, Matadi na Popokabaka chini yake.
Askofu mkuu wake ni kardinali Fridolin Ambongo Besungu, O.F.M.Cap.