Jimbo Kuu la Songea (kwa Kilatini Archidioecesis Songeana) ni mojawapo kati ya majimbo makuu 7 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, likiongoza majimbo ya kusini, yakiwemo Mbinga, Tunduru-Masasi, Mtwara, Lindi na Njombe.
Makao makuu ni mjini Songea, ambapo pana Kanisa kuu la mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba.