John Anthony Boissonneau (alizaliwa 7 Desemba 1949, huko Scarborough) ni Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki katika Jimbo Kuu la Toronto, Kanada.
Alipadrishwa tarehe 14 Desemba 1974.[1]
Tarehe 23 Machi 2001, Papa Yohane Paulo II alimteua kuwa Askofu wa jimbojina la Tambeae na Askofu Msaidizi wa Toronto. Uwekwaji wake wakfu kama askofu ulifanyika tarehe 29 Mei mwaka huohuo, ukiongozwa na Kardinali Aloysius Ambrozic, Askofu Mkuu wa Toronto, huku wasaidizi wake wakiwa maaskofu wasaidizi wa Toronto Nicola De Angelis CFIC na Anthony Giroux Meagher.