John Magufuli | |
John Magufuli, 2015 | |
Muda wa Utawala 5 Novemba 2015 – 17 Machi 2021 | |
Waziri Mkuu | Kassim Majaliwa |
---|---|
Makamu wa Rais | Samia Suluhu |
mtangulizi | Jakaya Kikwete |
aliyemfuata | Samia Suluhu |
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
| |
Muda wa Utawala 17 Agosti 2019 – 17 Agosti 2020 | |
mtangulizi | Hage Geingob |
aliyemfuata | Filipe Nyusi |
Muda wa Utawala 28 Novemba 2010 – 5 Novemba 2015 | |
Waziri Mkuu | Mizengo Pinda |
mtangulizi | Shukuru Kawambwa |
aliyemfuata | Makame Mbarawa |
Muda wa Utawala Novemba 2000 – 21 Desemba 2005 | |
Waziri Mkuu | Frederick Sumaye |
aliyemfuata | Basil Mramba |
Muda wa Utawala 13 Februari 2008 – 6 Novemba 2010 | |
Waziri Mkuu | Mizengo Pinda |
mtangulizi | Anthony Diallo |
aliyemfuata | David Mathayo David |
Muda wa Utawala 6 Januari 2006 – 13 Februari 2008 | |
Waziri Mkuu | Edward Lowassa |
aliyemfuata | John Chiligati |
Muda wa Utawala Novemba 1995 – Julai 2015 | |
aliyemfuata | Medard Kalemani |
tarehe ya kuzaliwa | Chato, Tanganyika (saga Tanzania) | 29 Oktoba 1959
tarehe ya kufa | 17 Machi 2021 (umri 61) Dar es Salaam, Tanzania |
chama | Chama cha Mapinduzi |
ndoa | Janeth Magufuli |
watoto | 7 |
Military service | |
Allegiance | Tanzania |
Service/branch | Jeshi la Ulinzi la Wananchi |
Years of service | 1983–1984 |
John Pombe Joseph Magufuli (alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 - 17 Machi 2021) alikuwa rais wa tano wa Tanzania, akitokea katika chama cha Mapinduzi CCM. Aliongoza kwa muda wa miaka mitano na nusu hadi kifo chake[1].
Aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki katika bunge la kitaifa huko nchini Tanzania na tangu mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi.[2]
Tarehe 12 Julai 2015 alichaguliwa kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi akiwa na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan.
Tarehe 29 Oktoba 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kura 8,882,935 sawa na 58.46% pamoja na makamu wa rais Samia Suluhu Hassani.
Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama rais wa tano wa Tanzania, ingawa upinzani haukukubali matokeo hayo.
Baada ya uchaguzi wa tarehe 28 Oktoba 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza tena mshindi pamoja na makamu wa rais Samia Suluhu Hassan kwa kura 12,516,252 sawa na 84.4% ingawa kulikuwa na malalamiko makubwa[3].