Joseph Haydn (jina kamili Franz Joseph Haydn) alikuwa mtungaji wa muziki kutoka nchi ya Austria. Alizaliwa tarehe 31 Machi au 1 Aprili 1732 katika kijiji kikubwa cha Rohrau, jimbo la Austria Chini. Aliaga dunia tarehe 31 Mei 1809 mjini Vienna.
Amekuwa maarufu kwa jina la heshima la "baba wa simfoni". Wajerumani na Waaustria hasa wanamkumbuka kama mtungaji wa muziki wa wimbo uliokuwa wimbo wa taifa katika Milki ya Austria na baadaye kuwa wimbo wa taifa nchini Ujerumani hadi leo (wimbo wa Wajerumani).