Juliani wa Sora (alifariki Sora, Lazio, Italia, 161 hivi) alikuwa Mkristo aliyeuawa kwa kukatwa kichwa wakati wa dhuluma ya kaisari Antoninus Pius dhidi ya imani hiyo kwa kuwa alihubiri Injili akitokea Dalmatia (leo nchini Kroatia) na kuelekea Campania[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Wa kwanza wanaadhimisha sikukuu yake tarehe 27 Januari[2], wa pili tarehe 11 Agosti[3].