Jumba la Maajabu (kwa Kiarabu : Beit-al-Ajaib, بيت العجايب) ni jengo la kihistoria katika Mji Mkongwe, Zanzibar. Ni jengo kubwa na refu zaidi la Mji Mkongwe lililojengwa mnamo mwaka 1883 kwa amri ya Sultani Sayyid Bargash. Linatazama Bustani ya Forodhani kwenye ukingo wa bahari, karibu na boma la Wareno na ikulu ya zamani ya Sultani. [1] Jumba la Maajabu lilikuwa na Makumbusho ya Historia na Utamaduni wa Zanzibar hadi kufungwa kwa shughuli za matengenezo yaliyoanza mwaka 2019 kwa msaada kutoka Oman[2]. Tarehe 25 Desemba 2020 sehemu kubwa ya jengo iliporomoka.[3]