Jumla

Alama ya jumla.

Katika hisabati, jumla (kwa Kiingereza: addition) ni moja ya uendeshaji wa hesabu nne (pamoja na mgawanyiko, utoaji na dharuba). Jumla ni kinyume cha utoaji. Alama ya jumla ni "+".

Mfano wa 3+2=5 matofaa.

Kwa usahihi, jumla ni mchakato wa kujumlisha thamani ya namba moja na thamani ya namba nyingine. Kwa mfano, 3+2 = 5.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne