Jurawa | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Jurawa kaskazi (Passer griseus)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 5:
|
Jurawa ni spishi mbalimbali za ndege wadogo za jenasi Passer katika familia Passeridae ambao wanafanana na shomoro wenye kichwa kijivu. Ndege hawa wana domo fupi na nene lifaalo kula mbegu, lakini hula wadudu wadogo pia hasa wanapokuwa makinda. Spishi hizi zinatokea Afrika tu.