Kalenda ya Kiarmenia ni aina ya kalenda iliyoanzishwa nchini Armenia na kutumiwa na watu Waarmenia au wenye asili ya Armenia. Hesabu yake ya miaka ilianza 552 katika Kalenda ya Gregori.
Mwanzo wa mwaka hutokea wakati wa Julai. Ilikuwa ni kalenda ya jua lenye miezi 12 ya siku 30 na mwezi mmoja mfupi wa siku 5 au 6.
Kabla ya kuwa Wakristo Waarmenia walitumia hesabu ya miaka iliyoanza mwaka 2492 KK.