Kali Yuga

Kalki na farasi wake

Kali Yuga (Devanāgarī: कलियुग, lit. "Kipindi cha Kali" yaani "kipindi cha dhambi") ni kimoja cha vipindi vinne vya muda wa ulimwengu kufuatana na imani ya Uhindu.

Kufuatana na imani hii, ulimwengu baada ya uumbaji una muda wake maalumu unaogawiwa kwa "yuga" au vipindi vinne. Ulimwengu unaanza baada ya kila uumbaji katika yuga au kipindi cha kwanza ambako nguvu ya kimungu ya karma inapatikana kwa nguvu kwa hiyo dunia inajaa maadili mema. Kila yuga nguvu ya karma inapungua hadi katika kipindi au yuga ya nne nguvu ya karma na maadili iko robo moja tu. Pepo baya kwa jina "Kali" [1] anatawala yuga hii.

Kufuatana na maandiko ya Kihindu Kali Yuga hii ilianza 23 Januari 3102 BK. Wahindu walio wengi huamini yuga hii ina muda wa miaka 432,000. Imani hii inapatikana pia kati ya wafuasi wa Kalasinga[2]

  1. aliye tofauti na mungu wa kike anayeitwa Kali
  2. "The Guru Nanak (founder of Sikhism) Prophecies". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-06. Iliwekwa mnamo 2014-04-11.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne