Kalimba

Kalimba toka Afrika Kusini

Kalimba ni ala ya muziki toka Afrika hasa Kusini kwa Sahara. Kalimba inaundwa na ubao na mabamba membamba ya chuma, kwa hivyo ni ala ya mabamba (kwa Kiingereza: lamelophone). Kalimba zinaitwa pia likembe, ilimba, mbira huru, mbira njari, mbira nyunga nyunga, nhare, matepe, njari, sansu, zanzu, karimbao, marimba, karimba, okeme, ubo, sanza au gyilgo katika sehemu mbalimbali za Afrika.

Marimbula toka Visiwa vya Karibi alifanya kutia na kalimba toka Afrika.

Wanamuziki mashuhuri ambao hupiga kalimba au mbira ni Thomas Mapfumo toka Zimbabwe na Kinobe toka Uganda.

Muziki toka Zimbabwe

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne