Kampuni ya Sukari ya Mumias ni kampuni ya sukari nchini Kenya. Ina makao yake makuu mjini Nairobi na operesheni zake katika mji wa Mumias. Jina lake hufupishwa kuwa MSC. Mumias imesajiliwa katika Soko la Hisa la Nairobi.
Mumias hufanya kazi ya utengenezaji na uuzaji wa sukari. Kampuni hii hukuza miwa; mashamba yake yenyewe hutoa hadi asilimia 7 ya mapato yake ya mwaka. Lakini hupata nyingi ya miwa yake kutoka zaidi ya wakulima 50,000 waliosajiliwa kama "out growers" wakiwa na zaidi ya 400 km ² chini ya kilimo. Pia imekuwa kifua mbele katika uzalishaji wa mafuta ya mitende ya hali ya juu katika maeneo mbalimbali ambayo hapo awali yalidhaniwa kuwa baridi mno kwa kulima kibiashara, kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa FAO. Mwaka wa 2005 Mkurugenzi Mkuu Evans Kidero alitangaza mipango ya upanuzi na kuingilia uzalishaji wa ethanol ili kufaidika na gharama kubwa ya mafuta. Mumias iko katika Mkoa wa Magharibi katika eneo kijadi lilikwua makaazi ya kabila la Waluyia