Kamusi ya Kiswahili Sanifu (kifupi: KKS) ni kamusi ya lugha ya Kiswahili iliyotolewa mara tatu na wataalamu wa TUKI (sasa TATAKI) kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Inaorodhesha vidahizo (maneno) kwenye kurasa 646, pamoja na maelezo, orodha ya vibadala, kurasa za picha, jedwali za vivumishi na viwakilishi na orodha ya majina ya nchi.
Kamusi hii inakusanya maneno ya Kiswahili sanifu na kuyaeleza kwa lugha yenyewe ya Kiswahili, ikiongoza kwa Kiswahili sanifu.