Kani (kwa Kiingereza force) ni athira ya nje inayoweza kubadilisha hali ya utulivu au mwendo kwenye gimba. Hupimwa kwa nyutoni.[1]
Kani huwa na tabia za kiwango (ukubwa) na mwelekeo. Alama yake ni F.
Dhana ya kani iliundwa na Isaac Newton. Alisema katika kanuni yake ya pili kuwa :.
Hapo ni kani,
ni masi ya gimba,
na ni mchapuko wa gimba.
Fomula inasema ya kwamba kama kani iko juu ya gimba litakuwa na mwendo na mwendo huo utaongezeka zaidi na zaidi.
Kama kani ni dhaifu na masi ya gimba ni kubwa itachukua muda mwingi hadi gimba litapata mchapuko mkubwa. Lakini kama kani ni kubwa na masi ya gimba ndogo litakimbia haraka karibuni sana.