Kanisa Anglikana la Tanzania ( ACT ) ni jimbo la Jumuiya Anglikana Duniani. Makao makuu yake yako Dodoma. Lina dayosisi 28 ambazo ziko 27 Tanzania bara na 1 iko Zanzibar. Kila dayosisi huongozwa na askofu wake.
Hadi mwaka 1970, Waanglikana wa Tanzania walikuwa sehemu ya Jimbo la Afrika ya Mashariki pamoja na Kenya hadi kuanzishwa kwa majimbo ya pekee kila upande.
Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania tangu mwaka 2018 ni Maimbo Mndolwa. [1]