Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia

Kanisa kuu la Utatu mtakatifu, Addis Ababa.

Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia (kwa Kiamhara የኢትዮጵያ:ኦርቶዶክስ:ተዋሕዶ:ቤተ:ክርስቲያን, Yäityop'ya ortodoks täwahedo bétäkrestyan) ni madhehebu ya dini ya Ukristo iliyotawala watu wa jamii ya Waamhara kwa karne kadhaa hadi sasa.

Wakristo hao wanaotaka kuzingatia imani sahihi ni sehemu muhimu katika utamaduni wa Ethiopia na Eritrea[1].

Kwa sasa ni kubwa zaidi duniani kuliko mengine yote ya jamii ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki, likiwa na waumini milioni 45-50.[2] wengi wao wakiishi nchini Ethiopia,[3] lakini pia Mashariki ya Kati, Ulaya na Amerika.

  1. FDRE States: Basic Information - Amhara Ilihifadhiwa 10 Machi 2007 kwenye Wayback Machine., Population (accessed 26 Machi 2006)
  2. "Ethiopia: Orthodox Head Urges Churches to Work for Better World". Iliwekwa mnamo 2006-09-13.
  3. Berhanu Abegaz, "Ethiopia: A Model Nation of Minorities" (accessed 6 April 2006)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne