Kanisa la Kiorthodoksi la Siria ni mojawapo kati ya yale ya Waorthodoksi wa Mashariki.
Asili yake ni nchi za Siria, Uturuki na Iraq za leo, lakini kwa sasa waamini wengi zaidi wanaishi India au wametokea nchi hiyo. Wengi kati ya wale wa eneo asili walilazimika kuhama katika karne ya 20, wakaeneza imani na mapokeo yao duniani. Kwa jumla wako milioni moja unusu.
Tangu mwaka 1959 makao makuu yako Damasko.