Kanye West | |
---|---|
![]() Kanye West kunako mwaka 2007.
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Kanye Omari West |
Amezaliwa | 8 Juni 1977 Atlanta, Georgia, Marekani |
Asili yake | Chicago Illinois Marekani |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Mtayarishaji Rapa Mshairit Mtunzi wa nyimbo |
Ala | Sauti Ngoma Kinanda |
Studio | GOOD Music Roc-A-Fella Def Jam |
Ame/Wameshirikiana na | Child Rebel Soldier, Jay-Z, Common, Talib Kweli, Consequence, John Legend, Mos Def, Lupe Fiasco, Pharrell, GLC |
Tovuti | Kanyeuniversecity.com |
Kanye Omari West (amezaliwa tar. 8 Juni 1977)[1] ni mshindi mara ishirini na moja wa Tuzo za muziki za Grammy, akiwa kama rapa-mtayarishaji bora wa muziki kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Kanye West.
West alitoa albamu yake ya kwanza mnamo mwaka wa 2004, na albamu ilikwenda kwa jina la The College Dropout. Albamu yake ya pili iliitwa Late Registration na ilitoka mnamo mwaka wa 2005, na pia ikafuatia albamu yake ya tatu iliyotoka mwaka 2007 ikiwa na jina la Graduation.
Albamu zake zote tatu zilipata tuzo kadhaa, umaarufu,[2][3][4] na mafanikio ya kibiashara. West pia anamiliki studio yake mwenyewe iitwayo GOOD Music.[5] Wazazi wa West walitalikiana wakati akiwa na umri wa miaka mitatu, kisha yeye na mama yake wakaamia zao mjini Chicago, Illinois. Alijiandikisha katika Chuo Kikuu cha Chicago lakini baadaye aliacha kujiendeleza na masuala yake ya kazi za muziki.
Alianza kujibebea umaarufu baada ya kutengeneza single kadhaa za muziki. Miongoni mwa single alizofanya ni pamoja na ya Jay-Z, Alicia Keys, na Janet Jackson. Staili nyingi za West katika utayarishaji wake huwa anaweka vielelezo vya sauti vyembamba ambavyo vinaambatana na vigoma na ala tupu za muziki.