Kaprasi wa Agen (alifariki Agen, Akwitania, leo nchini Ufaransa, 303 hivi) alikuwa Mkristo aliyeuawa kwa ajili ya imani yake kutokana na dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1][2][3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Oktoba[4].