Kashmir (Kihindi: कश्मीर, Kiurdu: کشمیر) ni eneo katika kazkazini ya Bara Hindi kwenye milima ya Himalaya. Eneo hili limegawiwa kati ya Pakistan na Uhindi tangu 1947. Sehemu ndogo katika milima ya juu ya Kazkazini imevamiwa na Uchina tangu 1962.
Fitina ya Kashmir imesababisha tayari vita tatu za 1947, 1965 na 1999 kati ya India na Pakistan. Imekuwa pia chanzo cha ugaidi ndani ya Uhindi.