Katiba

Picha inayomwonyesha rais wa kwanza wa Marekani George Washington katika baraza la katiba la mwaka 1787 lililofanyika huko Marekani kwa mara ya kwanza.

Katiba ni sheria au kanuni zinazoaInisha jinsi ambavyo nchi, chama, au shirika vitakavyoendesha shuguli zao.

Kwa upande wa nchi, katiba ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba za nchi pia huainisha haki za msingi za wananchi.

Kuna aina kuu mbili za Katiba ambazo ni:

  • (a) Katiba isiyo ya maandishi (ya kimapokeo)
  • (b) Katiba ya maandishi.

Katiba ya India ndiyo katiba ndefu kuliko katiba yoyote duniani.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne