Kaunti ya Busia ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 893,681 katika eneo la km² 1,696.3, msongamano ukiwa hivyo wa watu 527 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Busia.
Shughuli kuu ya kiuchumi ni biashara na nchi jirani ya Uganda, pamoja na mji wa Busia kituo cha mpakani.
Mbali na mji, uchumi wa wilaya hutegemea sana uvuvi na kilimo, mazao msingi yakiwa pamoja na mihogo, mtama, viazi vitamu, maharagwe, na mahindi.
Wilaya ya Busia ni makao ya kabila la Waluhya nchini Kenya ambao wanapatikana hasa katika sehemu za Magharibi mwa Kenya.