Kaunti ya Kiambu | |||
---|---|---|---|
Kaunti | |||
![]() | |||
| |||
Kaulimbiu: "" | |||
Kiambu County in Kenya.svg![]() Kaunti ya Kiambu katika Kenya | |||
Nchi | ![]() | ||
Ilianzishwa | Machi 4th 2013 | ||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Kati | ||
Mji mkuu | Kiambu | ||
Miji mingine | |||
Serikali | |||
Gavana | Ferdinand Waititu | ||
Naibu wa Gavana | Dkt. James Nyoro | ||
Seneta | Kimani Wamatangi | ||
Mwakilishi wa wanawake | Gathoni wa Muchomba | ||
Bunge | Bunge la Kaunti ya Kiambu | ||
Spika | Stephen Ndichu[1] | ||
Wawakilishi Wadi | 60[2] | ||
Maeneo bunge | 12 | ||
Eneo | |||
Jumla | km2 2 538.6 (sq mi 980.2) | ||
Idadi ya Watu | |||
Jumla | 2,417,735 | ||
Msongamano | 952 | ||
Majira ya Saa | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||
Tovuti kiambu.go.ke |
Kaunti ya Kiambu ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Ilikuwa mojawapo ya wilaya za Kenya katika Mkoa wa Kati baada ya nchi kupata uhuru.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 2,417,735 katika eneo la km2 2,538.6, msongamano ukiwa hivyo wa watu 952 kwa kilometa mraba[3].
Kupakana na Nairobi kumeifanya iwe na idadi ya wakazi wengi mijini, kwa sababu ya maendeleo katika sekta ya mali yasiyohamishika. Sekta za viwanda na ukulima pia zimechangia kukuza kaunti hii kiuchumi.
Makao makuu ya kaunti hii ni mji wa Kiambu. Hata hivyo, utendaji wa kaunti hutekeleza majukumu yake kutoka Thika, ambayo wilaya yake imemezwa tena na Kiambu (2010).