Kaunti ya Kilifi

Kaunti ya Kilifi
Kaunti
Bendera Nembo ya Serikali
Kaulimbiu: ""
Kilifi County in Kenya.svg
Kaunti ya Kilifi katika Kenya
Nchi Kenya
Nambari3
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Pwani
Mji mkuuKilifi
Miji mingineMalindi
Serikali
GavanaAmason Jefa Kingi
Naibu wa GavanaGideon Edmund Saburi
SenetaStewart Mwachiru Shadrach Madzayo
Mwakilishi wa wanawakeGetrude Mbeyu Mwanyanje
BungeBunge la Kaunti ya Kilifi
SpikaJimmy Kahindi
Wawakilishi Wadi35
Maeneo bunge7
Eneo
Jumlakm2 12 539.7 (sq mi 4 841.6)
Idadi ya Watu
Jumla1,453,787
Msongamano116
Majira ya SaaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovuti
kilifi.go.ke

Kaunti ya Kilifi ni kaunti nchini Kenya katika eneo la Mkoa wa Pwani wa awali. Ilianzishwa mwaka 2010 kwa kuunganisha wilaya za Kilifi na Malindi.

Eneo lake ni km² 12,539.7. Eneo hilo lilikuwa na wakazi 1,453,787 wakati wa sensa ya mwaka 2019, msongamano ukiwa hivyo wa watu 116 kwa kilometa mraba[1].

Mji mkuu uko Kilifi lakini mji mkubwa zaidi ni Malindi.

Kiongozi wa serikali yake ni gavana anayechaguliwa na wananchi.

Eneo la kaunti liko upande wa kaskazini na kaskazini-mashariki ya Mombasa. Sehemu zinazotembelewa na watalii ni hasa Kikambala, Watamu, Malindi na Kilifi.

  1. www.knbs.or.ke

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne