Kaunti ya Mombasa

Kaunti ya Mombasa
Kaunti 001
Kaunti
Bendera Nembo ya Serikali
Kaulimbiu: "Utangamano kwa maendeleo"
Mombasa County in Kenya.svg
Kaunti ya Mombasa katika Kenya
Coordinates: 4°03′S 39°40′E / 4.050°S 39.667°E / -4.050; 39.667
Nchi Kenya
Nambari1
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Pwani
Mji mkuuMombasa
Miji mingine
Serikali
GavanaHassan Ali Joho
Naibu wa GavanaDkt. William Kingi
SenetaMohammed Faki
Mwakilishi wa wanawakeAsha Hussein Mohammed
BungeBunge la Kaunti ya Mombasa
SpikaArub Ibrahim Khatri
Wawakilishi Wadi30
MahakamaMahakama ya Rufaa, Mombasa
Maeneo bunge6
Eneo
Jumlakm2 219.9 (sq mi 84.9)
Idadi ya Watu
Jumla1,208,333
Msongamano5,495
Majira ya SaaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovuti
mombasa.go.ke

Kaunti ya Mombasa imeshika nafasi ya wilaya ya Mombasa baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010. Kaunti hii ni mojawapo ya kaunti mbili ambazo pia ni jiji na ndio kaunti ndogo kabisa kati ya kaunti zote.

Inapakana na kaunti za Kwale na Kilifi ambazo pamoja na kaunti za Mombasa, Lamu, Tana River na Taita Taveta zilikuwa zinatengeneza Mkoa wa Pwani.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,208,333 katika eneo la km2 219.9, msongamano ukiwa hivyo wa 5,495 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu ya serikali ya kaunti yako katika jiji la Mombasa.

  1. www.knbs.or.ke

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne