Kaunti ya West Pokot | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kaunti | |||||
![]() Wanawake Wapokot wakiwa Kapenguria, Pokot Magharibi | |||||
| |||||
Kaulimbiu: "" | |||||
West Pokot County in Kenya.svg![]() Kaunti ya West Pokot katika Kenya | |||||
Coordinates: 1°14′00″N 35°07′00″E / 01.23333°N 035.1167°E | |||||
Nchi | ![]() | ||||
Nambari | 24 | ||||
Ilianzishwa | March 4, 2013 | ||||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Bonde la Ufa | ||||
Mji mkuu | Kapenguria | ||||
Miji mingine | |||||
Serikali | |||||
Gavana | Prof. John Krop Lonyangapuo | ||||
Naibu wa Gavana | Dkt. Nicholas Owon Atudonyang | ||||
Seneta | Samuel Losuron Poghisio | ||||
Mwakilishi wa wanawake | Lilian Tomitom | ||||
Bunge | Bunge la Kaunti ya West Pokot | ||||
Spika | Catherine Mukenyang | ||||
Wawakilishi Wadi | 20 | ||||
Maeneo bunge | 4 | ||||
Eneo | |||||
Jumla | km2 9 123.2 (sq mi 3 522.5) | ||||
Idadi ya Watu | |||||
Jumla | 621,241 | ||||
Msongamano | 68 | ||||
Majira ya Saa | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||||
Tovuti http://westpokot.go.ke |
Kaunti ya West Pokot ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 621,241 katika eneo la km2 9,123.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 68 kwa kilometa mraba[1]..
Makao makuu yako Kapenguria.
Inajulikana kwa kuwa na bwawa la uzalishaji umeme la pekee lililo kaskazini mwa Bonde la Ufa liitwalo Turkwell. Pia, Makumbusho ya Kapenguria yapo katika kaunti hii, ambapo wapigania uhuru sita walikamatwa na kufungwa jela na serikali ya kikoloni wakati wa hali ya hatari mwaka 1952.