Keki ni chakula kinachotengenezwa kwa kuoka unga wa nafaka, maji au zaidi maziwa, sukari, soda ya kuokea pamoja na shahamu (k.m. siagi), na nyongeza nyingine kama vile mayai.
Jina latokana na neno la Kiingereza "cake" .
Keki zilianza kama mkate wa pekee ulioongezwa sukari au asali, baadaye pia shahamu au mafuta.[1]
Ilhali mwanzoni keki na mkate hazikutofautishwa sana baadaye mbinu za kuoka keki tamu ziliongezeka sana. Tangu karne ya 18 mafundi wa Ualya waliacha kutumia hamira kama mbinu wa kupata keki laini badala yake walitumia yai lililopigwa hadi kuwa pofu; katika karne ya 19 elimu ya kemia iliunda matumizi ya soda ya kuokea ambayo ni kabonati natiri (magadi) inayotoa gesi wakati wa kuoka na hivyo kuunda nafasi ndani ya kinyunga.[2]
Siku hizi kuna aina maelfu za keki.