Kenelmi (pia: Kenelm au Cynehelm; alifariki 812/821) alikuwa mwana wa mfalme wa Mercia (leo nchini Uingereza)[1] aliyeheshimiwa sana katika Karne za Kati[2].
Hadi leo anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Julai[3].