Kiacipa-Magharibi ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Waacipa. Mwaka wa 1995 idadi ya wasemaji wa Kiacipa-Magharibi imehesabiwa kuwa watu 20,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiacipa-Magharibi iko katika kundi la Kikainji.