Kiadi (pia Kibori) ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uhindi inayozungumzwa na Waadi. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kiadi imehesabiwa kuwa watu 97,000. Pia kuna wasemaji 1090 nchini Uchina (1999); pale huitwa Kiluoba ya Boga'er na wasemaji wake huitwa Waluoba. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kiadi iko katika kundi la Kitani.