Kiadnyamathanha

Kiadnyamathanha ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Waadnyamathanha kwenye makao ya Nepabunna katika jimbo la South Australia. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kiadnyamathanha ilihesabiwa kuwa watu 107, yaani lugha iko hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiadnyamathanha kiko katika kundi la Kiyura.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne