Kiakwa

Kiakwa ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Kongo inayozungumzwa na Waakwa. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiakwa imehesabiwa kuwa watu 24,100. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiakwa iko katika kundi la C30.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne