Kialago

Kialago ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Waalago. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kialago imehesabiwa kuwa watu 35,100. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kialago iko katika kundi la Kiidomoidi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne