Kiamba ni lugha ya Kibantu nchini Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Waamba. Ni nchini Uganda ambako wengi wa wasemaji wa Kiamba hukaa. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kiamba katika Jamhuri imehesabiwa kuwa watu 4500. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiamba iko katika kundi la D30.